MUHOGO SASA KUUZWA CHINA KWA DOLA. - Rhevan Media

MUHOGO SASA KUUZWA CHINA KWA DOLA.




Serikali imepata soko nchini China, kupeleka tani 2 milioni za mihogo zenye thamani ya Dola 300 milioni za Marekani.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masalla (CCM). Ametaka kufahamu jitihada za Serikali katika kuwatafutia wakulima nchini masoko ya mazao yao. 
Akijibu swali hilo, Mwijage amesema mbunge huyo amewahisha masuala ya bajeti ijayo na kwamba, Serikali tayari imepata soko la mihogo nchini China.
Awali, Mbunge wa Viti Maalumu, Hamida Mohamed Abdallah (CCM) ametaka kujua Sera ya Maendeleo Endelevu.
ya Viwanda ya Mwaka 1996-2020, jinsi inayolenga kuvifanya viwanda vya usindikaji mazao kuongeza thamani na kukuza uchumi.     

Previous
Next Post »