UTUMBUAJI MAJIPU UNAENDELEA MHANDISI WA MAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA KITANZINI . - Rhevan Media

UTUMBUAJI MAJIPU UNAENDELEA MHANDISI WA MAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA KITANZINI .

Mhandisi wa maji katika halmashauri ya wilaya ya Rorya Bw Emmanuel Masanja, amekamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya hiyo baada ya kutuhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia moja zilizolewa na ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya ukarabati wa mradi wa maji katika mji mdogo wa Shirati wilayani humo.
Akizungumza baada ya Mhandisi huyo wa idara ya maji kukamatwa na kukabidhiwa kwa jeshi la polisi na taasisisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini Takukuru wilayani Rorya, mkuu wa wilaya ya Rorya Bw Felix Lyaniva, amesema baada mkuu wa mkoa kufanya ziara wilayani humo, uongozi wa wilaya umebaini mkuu huyo wa idara ya maji kuhusika na ubadhilifu huo wa kiasi hicho cha fedha na hivyo kusababisha wananchi wa mji wa Shirati kukosa huduma ya maji kwa muda mrefu.
Katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali wilayani Rorya, mkuu wa mkoa wa Mara Bw Magesa Mulongo, amesema lazima hatua za haraka zikiwemo za uchunguzi zifanyike katika kuwezesha wahusika wote wa ubadhilifu huo wanakamatwa na hatua kali zichukuliwe dhidi yao.
Previous
Next Post »