BOKO HARAMU MARA NYINGINE HUWAZAMISHA WATOTO KUENDESHA MASHAMBULIZI. - Rhevan Media

BOKO HARAMU MARA NYINGINE HUWAZAMISHA WATOTO KUENDESHA MASHAMBULIZI.

Image copyrightBOKO HARAM VIDEO
Image captionBoko Haram mara nyingi huwazamisha watoto kuendesha mashambulizi ya kujitoa mhanga
Umoja wa mataifa unasema kuwa kutumiwa kwa watoto kama washambuliaji wa kujitoa mhanga na kundi la wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria, imeongezeka tangu mwaka uliopita.
Shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF linasema kuwa watoto 44 walitumiwa kufanya mashambulizi kama hayo nchini Cameroon, Chad na Nigeria mwaka uliopita, ikilinganishwa na watoto wanne waliotumiwa mwaka 2014.
Inaripotiwa kuwa washambuliaji watano wa kujitoa mhanga sasa ni watoto huku robo tatu wakiwa na wasichana.
UNICEF inasema kuwa wasichana hao wakati mwingine huleweshwa, kisha hufungwa milipuko kwenye miili yao na kulazimishwa kufanya mashambulizi.
Previous
Next Post »