Waziri wa Nishati wa Kenya, Cherles Keter, na ujumbe wake amezuiwa kuingia katika bandari ya Tanga.
Kutokana na hatua hiyo, serikali mkoani Tanga imetoa ufafanuzi kuhusu kuzuiwa kwa waziri huyo na ujumbe wake wa watu 13 kuwa kulitokana na kutokuwa na taarifa za ujio wao.
Keter na maofisa wake wandamizi wakiwamo makatibu wakuu, walijipenyeza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni.Ujumbe wa waziri huyo aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya nchi hiyo, Joseph Njoroge na mwenzake wa masuiala ya petroli, Andrew Kamau.
Vigogo hao, waliokuwa wameongozana na maofisa mbalimbali akiwamo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Usafirishaji wa Mafuta kutoka Lamu- Sudan Kusini- Ethiopia (Lappset), Sylvester Kasuku, walizuiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Tanga, baada ya kuwasili. Muloni na ujumbe wake, alitokea Kenya baada ya kukagua Bandari za Lamu na Mombasa na aliingia nchini kukagua Bandari ya Tanga, ikiwa hatua ya mchakato wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Ziwa Albert, Uganda hadi Bahari ya Hindi.
Sign up here with your email