MFALME WA SAUDI ARABIA AMDOKEZA NENO RAIS MAGUFULI. - Rhevan Media

MFALME WA SAUDI ARABIA AMDOKEZA NENO RAIS MAGUFULI.





Mfalme wa Saudi Arabia, Salman Bin Abdulaziz Al Saud amemhakikishia Rais John Magufuli, kuwa nchi yake imeichagua Tanzania kuwa nchi ya kipaumbele katika mpango wake wa kuimarisha zaidi mahusiano na Afrika uliolenga kuendeleza na kukuza biashara, uwekezaji na kushiriki katika miradi ya maendeleo.
Ujumbe wa Mfalme Salman uliwasilishwa kwa Rais Magufuli jana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Adel Al Jubeir Ikulu jijini Dar es Salaam. Katika salamu hizo pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuiongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania, Mfalme Salman Bin Abdulaziz Al Saud amesema Saudi Arabia imedhamiria kukuza zaidi mahusiano kati yake na Tanzania ili kuwaletea manufaa makubwa wananchi.
Previous
Next Post »