Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec), jana aligeuka kuvutio kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliohudhuria sherehe za kumuapisha Rais Dk. Ali Mohammed Shein, katika Uwanja wa Amani mjini hapa.
Jecha ambaye kuingia na kutoka kwake uwanjani hapo hakukutangazwa kama ilivyokuwa kwa viongozi wa kitaifa, aliwavutia wanachama hao baada ya kuteremka kutoka jukwaa kuu na kuelekea sehemu iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya kumuapishia Dk. Shein.Mwenyekiti huyo kwa sasa amekuwa kivutio kwa wananchi wengi hususan wanachama wa CCM baada ya kufuta uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
Jecha ambaye alikuwa amevalia vazi la kanzu, alionekana mpole wakati akishuka jukwaani na alipofika chini, ndipo wananchi hao walipoanza kumshangilia.Kiongozi huyo tangu alipotangaza kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huo mwaka jana kwa madai kwamba ulitawaliwa na kasoro nyingi, amekuwa haonekani hadharani.
Sign up here with your email