DENI LA TAIFA KUJADILIWA NA KAMATI ZA BUNGE. - Rhevan Media

DENI LA TAIFA KUJADILIWA NA KAMATI ZA BUNGE.





kujadili Deni la Taifa na kuagiza kukutana na idara na taasisi sita, zinazohusika na deni hilo.Uamuzi huo wa kamati ulifikiwa jana jijini Dar es Salaam wakati Kamati hiyo ilipokutana na Wizara ya Fedha na Mipango, kujadili taarifa yao ya fedha kwa mafungu tofauti.Idara na taasisi hizo ni Idara ya fedha za Nje, Idara ya Sera na Uchambuzi, Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tume ya Mipango na Ofisi ya Msajili wa Hazina.Akitoa uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hillary, alisema kamati hiyo haiwezi kujadili na Wizara ya Fedha, Deni la Taifa kama ambavyo linaonesha katika kifungu kinachotakiwa kujadiliwa, kwa sababu, wizara hiyo inaelekezwa kulipa tu.“Tumeshindwa kujadili Deni la Taifa na Wizara ya Fedha leo (jana), hawa wanapokea maelezo ya kulipa tu, hawajui vyanzo vya madeni vimetokea wapi, sasa tumeona tukutane kwanza na hizo idara na taasisi husika watuambie chanzo na deni likoje,” alisema Hillary.
Previous
Next Post »