Staa wa Muziki wa Bongo Flava, Ali kiba, amefunguka ya moyoni na kudai kuwa anatamani kufanya kazi na Maproducer wa Kitambo kwenye sanaa Tanzania, Master Jay wa MJ Records na P Funk Majani wa Bongo records.
Akizungumza, Kiba amesema hakuwahi kufanya nao kazi ndio maana ana hamu nao sana na mashabiki wategemee ngoma mbili atakazofanya na wakongwe hawa.
“Kiukweli Master Jay na P funk natamani sana kupiga nao kazi, na naahidi kuwatafuta na kufanya nao kazi, kwa hiyo fans wangu wategemee kazi nzuri ntakazofanya nao” alisema.
Katika ‘line’ nyingine King kiba amedai, anamkumbuka sana pia producer aliyetengeneza kazi zake kadhaa, KGT kwa sababu alikuwa ni zaidi ya mwalimu wa muziki kwake.
Sign up here with your email
