TIMU YA ARSENAL YAKOSA USHINDI. - Rhevan Media

TIMU YA ARSENAL YAKOSA USHINDI.



Matumaini ya Arsenal kutwaa taji la ligi ya Uingereza kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 12 yalipata pigo baada yao kulazwa 2-1 na Swansea uwanjani Emirates.
Arsenal walikuwa wakiongoza, kupitia bao la Joel Campell na ilionekana kana kwamba wangepunguza mwanya kati yao na viongozi Leicester.
Lakini Swansea, waliokuwa bila meneja wao Francesco Guidolin, walisawazisha kupitia Wayne Routledge.
Olivier Giroud na Alexis Sanchez waligonga mwamba wa goli lakini bahati haikusimama.
Ashley Williams aliwaadhibu na kufungia Swansea bao la ushindi na mwishowe Arsenal wakalazimishiwa kichapo cha 2-1.
Arsenal sasa wamo alama sita nyuma ya viongozi wa ligi Leicester City.
Previous
Next Post »