WAFANYAKAZI WA TRL WATISHIA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU. - Rhevan Media

WAFANYAKAZI WA TRL WATISHIA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU.



Wafanyakazi wa taasisi ya reli ya Tanzania na Zambia wametoa siku saba kwa uongozi wa reli hiyo kuwalipa mishahara yao ya kuazinia mwezi Januari hadi Juni mwaka 2015 na kuwa kama uongozi hautafanya hivyo watafanya maamuzi magumu.
Katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa reli Bwana Boaz Nyakewe lkplllpjijini Dar es Salaam amesema uamuzi huo umekuja baada ya ukimya unaoendele kufanywa na uongozi wa taasisi hiyo bila kujali jasho la wafanyakazi na ugumu wa maisha na kubaini wamekuwa siku zote wanazofanya kazi uongozi haujawahi kuwashirikisha mapato wala matumizi ya fedha zinazoingia na kutaka serikali iingilie kati mgogoro huo.
Akizingumzia kauli ya serikali ya kufuta ruzuku kwa baadhi ya taasisi na mashirika yake ili yajiendeshe yenyewe katibu huyo kwa niaba ya wafanyakazi wa reli wamesema ni vyema serikali ikaziwezesha taasisi hizo ikiwemo TRL kifedha na kuijengea uwezo wa kujiendesha badala ya kufuta ruzuku kwani kwa kufanya hivyo watawaumiza wafanyakazi wa chini.
Hata hivyo jitihada za ITV za kuutafuta uongozi wa reli ili kuzungumzia sakata hilo zimegonga mwamba baada ya kufika ofisini kwao na kuwakosa na jitiohada zaidi zinaendelea kufanyanywa.
Previous
Next Post »