MSANII AFUNGUKA KUHUSU ELIMU YA TANZANIA. - Rhevan Media

MSANII AFUNGUKA KUHUSU ELIMU YA TANZANIA.


Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Niki wa Pili kutoka katika kundi la Weusi amefunguka na kusema kuwa maendeleo ya Sayansi na Teknlojia nchini ni ndoto na kusema labda kama ni maendeleo ya followers kwenye mitandoa ya kijamii.Niki wa Pili amesema haya kufuatia idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha nne kufeli mitihani yao huku kukiwa na asilimia ndogo ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani hiyo na mbaya zaidi asilimia ndogo zaidi ya wanafunzi waliofaulu mitihani ya hesabu.
"Pale unaposkia 2.7% ndio waliopata division one, na 16% tuu ndio wamefaulu hesabu na 76% wamepata division zero na four...Unatambuwa kuwa maendeleo ya sayansi na technolojia ni ndoto.......labda maendeleo ya followers insta, snap chati...na comments nyingi kwenye page za watu maarufu(wa kiki)" Aliandika Niki wa pili.
Katika hatua nyingine msanii huyo amesema matokeo ya muundo huo ni yenye kulenga kutengeneza umasikini kwa wanafunzi kwani watu watashindwa kujikomboa kupitia elimu, kutokana na kufeli kwao jambo ambalo kama serikali ingeweka msingi mizuri na kuwekeza kwenye elimu ingesaidia nchi kufika mbele zaidi kimaendeleo, na wanafunzi wasingeweza kufeli kwa kiasi kikubwa na kuangamia kama hali ilivyo sasa nchini.
"Hongereni ACT Wazalendo kwa kujaribu kuliongelea swala hili la elimu nchini. Nchi imekaa kimyaa watoto wanaangamia na mbegu ya umaskini inapandwa." Aliandika Niki wa pili.
Previous
Next Post »