MSANI LULU ATOA TAMKO BAADA YA KUZUSHIWA. - Rhevan Media

MSANI LULU ATOA TAMKO BAADA YA KUZUSHIWA.


Msanii machachari anayefanya poa kwenye runinga za bongo kupitia filamu Elizabeth Michael au Lulu, amemuwakia mtu aliyepost kuwa amefariki na kuwataka watu wakaone picha za msiba wake, na kusema hafi mpaka siku za kwenye biblia ziishe.Kwenye ukurasa wake wa instagram Lulu ameandika maneno hayo huku akionyeshwa kuchukizwa na kitendo hicho cha kuzushiwa kifo, na kujisifia kuwa ana jina maarufu.
"Nasikia Nimekufa, wewe uliye Post hii Kama wewe utakuwepo tutaonana tena 2017 Inshaallah, halafu jifunze na kuandika Elizabeth vizuri kwanza (Niki report live kutoka heaven), this shows how jina langu lina KiKi, nishasema mniache jamani, kufa ntakufa sikatai lakini mpaka nimalize miaka iliyoandikwa kwenye biblia", aliandika Lulu.
Maneno hayo ya Lulu yameibua hisia za watu na kumjia juu mtu aliyepost taarifa hiyo kwenye mitandao, huku wakimtaka Lulu kutopigizana nao kelele kwani yeye ni kioo cha jamii hivyo ni kawaida kwa kuzushiwa taarifa za uongo.
Previous
Next Post »