MARAIS WATANO WAUVALIA NJUGA MGOGORO WA BURUNDI - Rhevan Media

MARAIS WATANO WAUVALIA NJUGA MGOGORO WA BURUNDI


Ujumbe wa Marais 5 wa Afrika umewasili Burundi jana katika jitihada za kujaribu kutanzua mgogoro wa kisiasa nchini humo uliodumu kwa zaidi ya miezi 10 na kushuhudia mauaji ya watu zaidi ya 400 huku zaidi ya raia 250,000 wakilazimika kutoroka.


Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zouma ndiye anaongoza ujumbe huo akiwa na Marais Macky Sall wa Senegal, Raisi wa Mouritania Mohamed Ould Abldel Azzi, Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba na waziri Mkuu wa Ethiopia Haile mariam Desalegn.
Kulingana na ratiba, viongozi hao wa Afrika watakutana na wadau mbali wa siasa za Burundi ikiwa ni pamoja na wakuu wa vyama vya kisiasa, wawakilishi wa asasi za kiraia, wakuu wa dini na madhehebu kabla ya kuwa na mazungumzo na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Awali Muungano wa Afrika uliazimia kutuma vikosi 5000 vya vya walindamani nchini humu , lakini kutokana na upinzani mkali wa serikali ya Burundi, AU ikaachana na mpango huo.
Kwa sasa Marais hao watakuwa na shughuli ya kuishawishi serikali kuketi meza moja na upinzani na kufufua mazungumzo jumuishi ambayo yalikwama tangu mwezi disemba licha ya kuzinduliwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda mwezi disemba mwaka jana baada ya serikali kupinga kujadiliana na sehemu moja ya wapinzani kwa madai kwamba wamesimamia vurugu nchini.
Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Maite Nkoana Mashabane ameelezea matumaini makubwa.
" Tuko hapa kuunga mkono Rais Zuma na marais wengine wanne wanaounda Ujumbe huu wa ngazi ya juu kuweka msukumo mchakato wa amani unaoendelea. Tangu tulipofika tumeona kwamba kuna hatua fulani iliofikiwa na kwamba kuna utashi wa kuendeleza mchakato huu. Ujumbe tumekuja nao ni ujumbe wa amani.
Tunaunga mkono kile chote kinacholeta amani na usalama, lakini kwa kuzingatia nini warundi wenyewe wanahitaji kama uungwaji mkono."
Previous
Next Post »