
Kampuni za vinywaji baridi ya Coca Cola pamoja na kampuni nyingine za vinywaji baridi zimetoa vifaa tiba zaidi ya aina 50 vyenye thamani ya shilingi bilioni kumi kwa bohari kuu ya dawa nchini Tanzania MSD.
Akizungumza Mara baada ya kupokea vifaa hivyo waziri mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema msaada huo unalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya katika hospitali zote za umma nchini ikiwa ni pamoja vituo vidogo vya afya na hospitali za rufaa.
Akimkaribisha waziri mkuu kuzumgumza, mara baadavya makabidhiano hayo katibu mkuu wa wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Dkt. Mpoki Ulusubisya amesema msaada huo wa vifaa tiba utakuwa chachu ya kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.
Mwenyekiti wa bodi ya bohari kuu ya dawa nchini Tanzania MSD, Prof. Idris Mtulia amesema kampuni hizo za vinywaji baridi zimeungana pamoja kuokoa maisha ya watanzania wengi wanaopoteza maisha kutokana na ukosefu wa vifaa tiba.
Sign up here with your email