MAGUFULI ANAONGEA SANA, KULIKO KASI YA VITENDO! - Rhevan Media

MAGUFULI ANAONGEA SANA, KULIKO KASI YA VITENDO!





JPM ni Rais maarufu "A Popular President", lakini anaongea hata kauli zisizopaswa kutolewa na Mkuu wa nchi wa karne ya sasa "A modern président"! Uchaguzi umeshakwisha - viapo na kauli za kukamia kuwa nchi hii ni tajiri sana na haipaswi kuwa masikini azigeuze kuwa vitendo badala ya kuendelea kuzipigia kampeni wakati yeye ndo amekabidhiwa jukumu la kuufanya utajiri huo wa nchi uhamie vijijini, mijini na majumbani mwa wananchi.
Hadi sasa tumefanikiwa kwenye "utumbuaji wa vijipu". Majipu makubwa hayajaguswa. Lakini pia - Mwaka 2020 kura hazitapigwa kwa kuangalia "vijipu"/majipu yalitumbuliwa kiasi gani bali kwa kutizama maisha ya wananchi yamebadilika kiasi gani? kilimo kimeboreshwaje? vijana na ajira? elimu na afya? miundombinu? uchumi? Mishahara ya wafanyakazi? Miuondombinu ya kazini? Madini yametusaidije? n.k.
Kwa wanaofuatilia siasa za dunia ya leo wanajua kuwa ni vigumu ku-transform nchi kupitia mfumo na watu walewale ndani ya miaka mitano. Huwenda unahitaji miaka 25 kufanya hivyo. Ndiyo maana, hivi vyama ambavyo Magufuli anaviita "vya hovyo", vitakuwa na ajenda na nguvu kubwa dhidi ya serikali ifikapo 2020, nadhani hataamini na huwenda akaingia kwenye "confusion and frustration".
Tusije kushangaa inafika 2020 mwalimu analipwa laki tatu na rais anahubiri nchi ni tajiri sana. Madawa hakuna hospitali na rais anahubiri hilo halitatokea kwenye utawala wake, watoto wanakaa chini na rais anaendelea kudai nchi ina misitu. Uongozi wa juu wa nchi siyo 1 jumlisha 1.
Mtatiro J.
Previous
Next Post »