MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imeanza kutekeleza jukumu la kukusanya kodi kwenye michezo ya kubahatisha jukumu ambalo ilikabidhiwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu
Akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam, Richard Kayombo, Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi amesema kwamba kutokana na nmabadiliko hayo TRA itakusanya kodi katika michezo yote ya kubahatisha ikiwemo casino, sports betting, slot machines, lottery na kupitia ujumbe mfupi wa kwenye simu (sms).
“Mshindi katika bahati nasibu atakatwa asilimia 18 ya kiasi alichoshinda na kuwasilishwa TRA na mchezaji bahati nasibu huyo na kwa upande wa wachezeshaji kuwasilisha asilimia ya mapato, casino 15%, sports betting 6%, SMS na lottery 30%, National lottery 10% na vslot machines ni 32,000/- kila mwezi.” Kayombo Aliongeza.
TRA ikishirikiana na bodi ya michezo ya kubahatisha imetoa na inaendelea kutoa mafunzo kwa wananchi na waendeshaji wa michezo hiyo na piainatoa wito kwa wahusika wote kutoa ushirikiano ili kufasnikisha ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi.
Sign up here with your email