RATIBA LIGI KUU KUFUMULIWA TENA - Rhevan Media

RATIBA LIGI KUU KUFUMULIWA TENA



Dar es Salaam. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/2018, itafanyiwa marekebisho makubwa kutokana na makosa yaliyojitokeza katika ratiba ya sasa.
Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao alisema kuwa ratiba ya sasa ina mapungufu mengi ambayo huenda yangeivuruga ligi hapo baadaye.
"Tulijipa kazi ya kuangalia ratiba iliyopo sasa na tukabaini kuna vitu vingi havikuzingatiwa mfano kalenda ya mashindano ya kimataifa.
Shirikisho tumeamua kuunda jopo la wataalamu wanne ambao watatuandalia ratiba itakayozingatia.
"Tuliwapa mamlaka bodi ya ligi kama njia ya kuelekea kuifanya bodi ijitegemee lakini kwa hili lililotokea la ratiba kubadilishwa, kuanzia sasa ratiba yoyote kabla haijatolewa ni lazima katibu mkuu wa TFF aione na kutia saini,”                       
Kidao aliongeza “tunapobadilisha ratiba tunawakwaza watu mbalimbali. Ratiba hii itafanyiwa tena mabadiliko kwa sababu kuna baadhi ya vitu havikuzingatiwa.”
Previous
Next Post »