UBOMOAJI WALIOJENGA KWENYE VYANZO VYA MAJI USIBAGUE - Rhevan Media

UBOMOAJI WALIOJENGA KWENYE VYANZO VYA MAJI USIBAGUE

 Tokeo la picha la BOMOA BOMOA JANGWANI

Dodoma. Wataalamu wa mazingira wameagizwa kutofanya ubaguzi wanapobomoa nyumba za waliojenga karibu na vyanzo vya maji.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy aliyetaka kujua kwanini baadhi ya watu waliojenga ndani ya mita 60 kutoka Ziwa Tanganyika wameachwa tofauti na matakwa ya sheria.
"Wataalamu wetu wanapaswa kuacha (ubaguzi) double standards wanapotekeleza suala hili. Utekelezaji wa sheria lazima uwe sawa kwa watu wote," amesema Jaffo.
Ametahadharisha kwamba ziwa hilo lipo hatarini kutoweka kwani lilivyo sasa ni tofauti na miaka 20 iliyopita. "Wananchi wanapaswa kuelimishwa juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji," amesisitiza.

Previous
Next Post »