JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM,21Juni, 2017.
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Romanus Mbilinyi Hellela (mstaafu), kilichotokea tarehe 18 Juni, 2017 katika Hospitali ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mwili wa marehemu utaagwa rasmi tarehe 23 Juni, 2017 kuanzia saa 2:00 asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na mazishi yatafanyika saa 8.00 mchana katika makaburi ya Kinondoni.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi : 0756 716 085
Sign up here with your email