QATAR YAENDELEA KUSUSWA , RAIA WAKE WAPEWA WIKI MBILI KUFUNGASHA VIRAGO - Rhevan Media

QATAR YAENDELEA KUSUSWA , RAIA WAKE WAPEWA WIKI MBILI KUFUNGASHA VIRAGO

 Tokeo la picha la NCHI YA QATAR

Cairo. Siku moja baada ya mataifa matano ikiwamo Saudi Arabia, Yemen na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kusitisha uhusiano wa kimataifa na nchi ya Qatar, Misri nayo inafunga anga zake kwa ndege za Qatar.
Jana mataifa hayo yaliweka wazi uamuzi huo kwa kile walichodai kuwa Taifa hilo linashirikiana na magaidi.
Tangu jana, Saudi Arabia ilisema inafunga njia zote za uchukuzi na mawasiliano zinazoelekea Qatar ikiwamo ndege, ardhi na bandari.
Mashirika makubwa ya ndege ikiwemo Emirates na Etihad ni miongoni mwa yatakayositisha safari za anga nchini humo.
Misri nayo imeungana na mataifa hayo huku raia wa Qatar nchini Bahrain, Saudi Arabia na UAE wakipewa  wiki mbili kuondoka katika nchi hizo.
Wakati mzozo huo ukiendelea kushika kasi, Qatar imekana kuunga mkono ugaidi huku ikiomba mazungumzo ili kumaliza tofauti hizo.
Lakini Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni wa Qatar, Sheikh Mohammed Bin Abdulrahman al-Thani, alikimbia kituo cha Al Jazeera kuwa ndege zake zinatumia njia za kimataifa za baharini kwa safari za kimataifa.










Previous
Next Post »