Moshi. Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo unaagwa kwa mara ya pili na wafuasi wa Chadema pamoja na wananchi ambao hawakupata nafasi ya kumuaga siku ya jana katika viwanja vya Majengo mjini Moshi.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mazishi, Joseph Selasini amewataka wananchi na watu wote waliohudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Usharika wa Kiborloni kuacha kupiga picha mwili wa marehemu ili kutunza heshima yake.
Viongozi mbalimbali wameendelea kuwasili katika kanisa hilo wakiwemo viongozi wa Chadema na Mbunge wa Singinda Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu.
Awali wafuasi na wanachama wa Chadema walifurika nyumbani kwa Ndesamburo kwa ajili ya kuandamana kupelekwa mwili wake kanisani.
Mwili wa Ndesamburo umesaliwa nyumbani kwake kabla ya kupelekwa kanisani.
Sign up here with your email