NYATI AVAMIA KIJIJI NA KUJERUHI WATU SABA - Rhevan Media

NYATI AVAMIA KIJIJI NA KUJERUHI WATU SABA

Picha inayohusiana
Ofisa Wanyamapori wilayani hapa, John Lendoyan na Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Girihuda Gegasa kwa nyakati tofauti walisema tukio hilo lilitokea jana saa moja asubuhi.
Mganga wa Zahanati ya kijiji hicho, Elias Matobera aliwataja majeruhi kuwa ni Julius Kitasho (57), Peter Umeju (37), Flora Juma(6) na Bebina Juma (4).
Wengine ni Emmanuel Bomani, Gomini Mnada na mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina Yopa.
“Kati ya hao, watoto wawili na Peter nimewapa rufaa kwenda hospitali ya wilaya kwa ajili ya huduma zaidi, hao watoto mmoja ameumia kichwani na mwingine tumbo ambalo linazidi kufura,” alisema Dk Matobera.
Akizungumza kwa njia ya simu mmoja wa majeruhi, Kitasho alisema nyati huyo alionekana kijijini kwao saa 12 asubuhi kwenye shamba la mahindi baada ya watoto kwenda kujisaidia ndipo akawajeruhi.
Alisema walipiga kelele ndipo nyati huyo akakimbia. “Wakati anakimbia (nyati) nilikuwa napita kwenye kichaka, ndipo akanichota na pembe zake na kunirusha chini. Baada ya kudondoka alitaka kunikanyaga, mbwa wangu akatokea na kuanza kubweka, hapo aliniacha hivyo nikapata nafasi ya kujiokoa,” alisema.
Mama wa watoto waliojeruhiwa, Neema Miano alisema alikwenda shambani na kuwaacha watoto nyumbani. “Nilishangaa kupewa taarifa kuwa wamejeruhiwa na nyati,” alisema.
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Girihuida Gegasa alisema tukio hilo limesababisha taharuki kijijini hapo kwa sababu halijawahi kutokea.
Ofisa wanyamapori wilaya, John Lendoyani alisema askari wa Pori la Akiba la Ikorongo na Grumeti walikwenda eneo la tukio na kumuua nyati.







Previous
Next Post »