“MEYA JIJI LA TANGA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE WAJASIRIAMALI KWENYE KATA 27” - Rhevan Media

“MEYA JIJI LA TANGA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE WAJASIRIAMALI KWENYE KATA 27”

  Mstahiki Meya wa Jiji la
Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza na wakina mama wajasiriamali
kwenye kata ya Nguvumali wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo
ambayo aliyaandaa kwa ajili ya kukabiliana na fursa mbalimbali za
kujiwekeza kiuchum ambapo mafunzo hayo yatafika kwenye kata 27 za Jiji
hilo
 Baadhi ya wanawake
wajasiriamali katika Kata ya Nguvumali Jijini Tanga wakiwa kwenye
mafunzo hayo
WANAWAKE wajasiriamali Jiji la
Tanga wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya kuwajengea uwezo katika utengenezaji na ubinifu wa
bidhaa mbalimbali ili waweze
kujikwamua kichumi jambo ambalo litasaidia kuondokana na utegemezi kwenye jamii.
Mafunzo hayo ambayo yamekwisha kuanza katika kata ya Nguvumali yanatarajiwa kuwafikia wanawake
wajasiriamali 120 na baadae kuendelea
kwenye maeneo mengine katika Jiji la Tanga.
Akizungumza juzi wakati akifungua mafunzo hayo,Mstahiki Meya wa
Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha
Selebosi alisema mpango huo utasaidiakuwakomboa wanawake kiuchumi
lakini pia kuwaandaa na ujio wa miradi mikubwa miwili mkoani hapa ikiwemo wa bomba la mafuta
na kiwanda kikubwa cha
kuzalishia saruji.
Alisema pia licha ya kuwapa uelewa masuala hayo lakini namna bora
ya kuzitumia kwa malengo
yatakayokuwa na tija fedha wanazokopa kutoka kwenye taasisi za kibenki kwani baadhi yao
wanashindwa kutambua wazitumie
vipi na kuzirejesha.
“Utakuta wakina mama wajasiriamali wanakopa fedha kwenye taasisi mbalimbali kwa malengo ya kufanya
biashara lakini kutokana na kutokuwa
na elimu hivyo wanaishia kuzitumia kwenye mambo mengine na

kusababisha madeni
“Alisema.
“Lakini pia wanawake wajasiriamali wanapaswa kutumia fursa ya
mafunzo hayo kuweza
kujiongezea wigo mpana kwani ujio wa mradi wa bomba la mafuta wenzetu wanaokuja kutoka
nchini Uganda hivyo lazima waweze na
uwezo wa juu “Alisema.
Aidha pia alisema wanatumia nafasi hiyo kuwaandaa kwa kusaidia
ili waweze kujiandaa kwa
kuongeza uzalishaji wa kilimo cha mboga mboga na matunda ikiwemo uuzaji wa mayai.
Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Kata ya Nguvumali ,Saumu Omari mafunzo hayo
yamewaongezea maarifa ambayo wanaweza
kuyatumia ili kuweza kuongeza uzalishaji lakini pia kukabiliana

na soko la ushindani wa
bidhaa.
Alisema kupitia elimu hiyo ya ujasiriamali wanaweza kuona namna
gani bora ya kuanzisha na
kubuni miradi ya kuwainua kiuchumi kwa kuzitumia fursa zitakazo patikana
Previous
Next Post »