MBUNGE AWAAGA WAPIGAKURA WAKE ASEMA MIAKA MITANO INAMTOSHA - Rhevan Media

MBUNGE AWAAGA WAPIGAKURA WAKE ASEMA MIAKA MITANO INAMTOSHA




Mbunge wa Ulyankulu, John Kadutu (CCM) amewaeleza wapiga kura wake kuwa hatarajii kugombea tena nafasi hiyo kipindi chake cha miaka mitano kitakapoisha.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kaswa kilicho ndani ya makazi wa wakimbizi, Ulyankulu, Kadutu alisema anatimiza dhamira yake ya kuwa mbunge kwa awamu moja kwa vile aliweka nadhiri kuwa pindi likipatikana jimbo la Ulyankulu na yeye kuwa mbunge atakuwa kwa kipindi cha miaka mitano pekee.
 Kadutu alikuwa akijibu swali kutoka kwa Ndikuma Abiudi mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, aliyeeleza kuwa kuna tetesi kwamba hatagombea kipindi cha pili na kutaka kufahamu sababu za kutogombea tena.
"Unatakiwa uachie uongozi wakati watu bado wanakupenda siyo mpaka upigwe mawe au kuzomewa," alisema Kadutu.
 Kadutu ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo hilo alisema pamoja na kwamba hatagombea mwaka 2020 anaendelea kuwatumikia na kutimiza hadi zake kama alivyowaahidi.








Previous
Next Post »