ALICHOKISEMA RAIS MAGUFULI KUHUSU WABUNGE WAROPOKAJI - Rhevan Media

ALICHOKISEMA RAIS MAGUFULI KUHUSU WABUNGE WAROPOKAJI

Baada ya kupokea Ripoti ya pili ya mchanga wa madini Ikulu leo June 12, 2017 Rais Magufuli pia amezungumzia swala  ya Wabunge wanaoropoka bungeni

Rais  amemwambia Spika; "Nitakuletea huu mzigo ili muweze kuipitia kule kwa maslahi mapana ya taifa letu, kwa wale watakaokua wanaropokaropoka….. unaenda vizuri

"Tumia mbinu hiyohiyo ya kuwafanya wasiropokee Bungeni, waropokee nje na kule tutadili nao vizuri kwasababu wanapokua kule ndani wana kinga wanaweza wakatukana chochote, sasa kinga wanayoitumia vibaya bungeni kainyooshe wewe.

"Wawe wanatoka kule bungeni, ukishamfukuza hata mwezi mzima… atakuja aropokee huku, na mimi nakueleza waache waropokee huku nitadili nao, wala siwatishi lakini hatuwezi kuwa kwenye vita wewe unaanza kugeuka kupiga wale wanaokwenda mbele…. ni nafuu unyamaze ukalale

"Mimi muda wangu utapita, tena ningetamani kweli hata ingekua mwaka huu tu niondoke niwaachie na wengine niwe nachungulia tu, saa nyingine hulali usiku kucha unahangaika documents ziko nyingi… saa nyingine nauliza Mungu kwanini ulinipa hii kazi, ni kazi ngumu"

Previous
Next Post »