Malkia Elizabeth wa Uingereza amesema ni vigumu kuepuka majonzi kufuatia kile alichosema ni msururu wa majanga yaliyokumba taifa hilo hivi karibuni.
Katika ujumbe wa kuadhimisha rasmi siku yake ya kuzaliwa, malkia amesema watu wa nchi hiyo wameonyesha mshikamano licha ya changamoto zinazoikabili.
Serikali ya Uingereza imesema itafanya kila iwezalo kurejesha imani ya walioyonusurika mkasa wa mbaya wa motokayika jengo la Grenfel Tower mjini London.
Hii ni baada ya waziri mkuu Bi Theresa May,kuzomewa na waandamanaji waliyokuwa na ghadhabu. Watu thalathini wamethibitishwa kufariki katika mkasa huo.
Hotuba ya Malkia Elizabeth inafuatia shabulizi la kigaidi la mwezi uliyopita mjini Manchester na pamoja na lile la London Bridge.
Sign up here with your email