GABO AMKANA WEMA SEPETU - Rhevan Media

GABO AMKANA WEMA SEPETU

Gabo Amkana Wema Sepetu
Akiwa jana kwenye kipindi cha FNL cha EATV, Gabo aliweka wazi kuwa maneno ya kuzushiwa kati yake na malkia huyo wa filamu yalianza tu baada ya picha za wawili hao kuanza kusambaa ambazo zilikuwa zina mahadhi ya mapenzi na kuwejka wazi kuwa zilikuwa zimebeba maudhui ya filamu.
"Mimi na Wema ni kazi tu. Hakuna kitu cha tofauti ambacho tulikifanya au tulikianzisha tukiwa location kwa sababu mpenzi wake alikuwa anakuja nae mara zote ambazo tulikuwa tuna shoot. vipande vyote alikuwa na sisi bega kwa bega sasa hata kama ni hayo mahusiano tungeyaanzisha muda gani? Watu wasifikiri tofauti kwani ukaribu wangu na Wema Sepetu umezalisha filamu ya Kisogo ambayo tunaamini watanzania wataifurahia" alisema Gabo

Aidha Gabo amezungumzia filamu yake mpya kwa kusema amefanya tofauti kabisa na ilivyozoeleka kuwa na filamu ndefu yenye maudhui ya kawaida na kwamba sasa filamu zake zitakuwa ni fupi huku zikiwa na ujumbe unaoeleweka.
"Nimejitolea kuitetea sanaa, nitafanya kile ambacho jamii inahitaji. kwa sasa nimefanya filamu fupi zinazohitajika na jamii yaani fupi na zinazoeleweka. Filamu hizi zitakuwa zina dakika 30 tu. Ni bora kuhangaika kuboresha soko la ndani la filamu kuliko kuwaza kwenda kimataifa, nitaitetea sana nahua na yenyewe
Previous
Next Post »