VYAMA VYA WAFANYAKZI VYAMPIGIA MAGOTI RAIS MAGUFULI - Rhevan Media

VYAMA VYA WAFANYAKZI VYAMPIGIA MAGOTI RAIS MAGUFULI





Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania wilayani ya Handeni vimetoa tamko la kumuomba Rais John Magufuli kuangalia njia stahiki ya kuwatoa kazini watumishi wa umma waliobainika kuwa na vyeti vya feki  badala ya kuwataka kuondoka wenyewe.

Wakizungumza kwenye kikao cha tathimini ya sherehe za wafanyakazi za Mei Mosi zilizofanyika wilayani hapa makatibu na waratibu wa vyama huru vya wafanyakazi wilaya ya Handeni walisema ni kweli lipo kosa la kughushi vyeti ambalo ni kinyume cha sheria za utumishi wa umma lakini kwa muda walitumikia Serikali wapewe stahiki zao.

Issa Mwambuga mratibu wa Chama cha Wafanyakazi Serikali Kuu na Afya(TUGHE) Handeni alisema ni kweli walishirikishwa katika kutambua watumishi wa umma ambao wana vyeti vya kughushi na kukutwa wanavyo hivyo ni vyema sasa Serikali iangalie ni jinsi gani ya kuwatoa kwa kupata stahiki zao.
Hamisi Ngomero Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Handeni alisema kilichotokea ni aibu kwa watumishi lakini hatua stahiki lazima zifanyike kwani wapo waliojiunga kwenye mifuko ya kijamii na fedha zao zipo  huko na wanatakiwa kupewa.







Previous
Next Post »