UKIMYA WATAWALA SHULE YA LUCK VICENT - Rhevan Media

UKIMYA WATAWALA SHULE YA LUCK VICENT


Arusha.Wakati wanafunzi  watatu majeruhi katika ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent  wakienda kwa matibabu nchini Marekani wanafunzi waliobaki shuleni leo wataendelea na masomo huku kukiwa na ukimya shuleni hapo.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Ephraim Jackson alisema jana kuwa shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa kesho baada ya kufungwa kwa wiki moja.
Amesema ratiba masomo pia itapangwa kesho ikiwepo siku za kuanza mitihani ya muhula.
Hata hivyo tofauti na siku nyingine jana shule katika shule hiyo kilikuwa kimya hakukuwa na mwanafunzi.
Baadhi ya wafanyakazi eneo la usafi wa madarasa na magari walikuwa wakiendelea na usafi.

Previous
Next Post »