UKATA WAIKABILI HOSPITALI YA MLOGANZILA - Rhevan Media

UKATA WAIKABILI HOSPITALI YA MLOGANZILA



Ukata waikabili hospitali ya Mloganzila
Sharon Sauwa, Mwananchi
Dodoma. Hospitali ya Kufundishia na Kutoa Huduma za Afya ya Mlongazila mkoani Dar es Salaam inakabiliwa na ukata baada ya Serikali kutopeleka fedha zilizotengwa katika bajeti ya kununulia dawa na vitenganishi iliyopitishwa na Bunge kwa ajili ya mwaka 2016/17.
Mwaka jana hospitali hiyo iliidhinishiwa na Bunge Sh 14.54 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vitenganishi na matumizi mengine lakini hadi kufikia Machi 21 mwaka 2017 ilikuwa haijapewa fedha hizo.
Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mbunge wa Nzega ambaye ni pia ni mjumbe wa kamati hiyo, Hussein Bashe amesema waziri aliiahidi kamati kuwa hadi kufikia Aprili Serikali itakuwa imetoa Sh 5 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.
 “Pamoja na changamoto ya fedha, bado chuo kina upungufu wa raslimali watu kwani mahitaji ni watumishi 900 na mpaka kamati inatembelea (Machi 21) walipatikana watumishi 381 tu sawa na asilimia 42.3 ya mahitaji yote,”amesema.

Previous
Next Post »