RAIS MPYA KOREA KUSINI AHOJI MAKOMBORA YA MAREKANI - Rhevan Media

RAIS MPYA KOREA KUSINI AHOJI MAKOMBORA YA MAREKANI



Rais Moon Jae-In 
Rais Moon Jae-In  

Seoul, Korea Kusini. Siku moja baada ya Korea Kusini kumchagua Moon Jae-In kuwa rais wa nchi hiyo, aliapishwa jana kuanza majukumu yake na mara akatoa wito haja ya kupunguza uhasama na jirani zao Korea Kaskazini.
Mbali ya kutoa wito huo, Moon alihoji kwa nini Marekani iliweka makombora ya ulinzi maarufu kama THAAD katika ardhi ya nchi yake.
Wakili huyo wa zamani wa haki za kibinadamu anayejulikana kwa maoni yake huria anataka kuimarisha uhusiano na Korea Kaskazini kinyume na sera iliopo kwa sasa. Amesema kuwa angependelea kutembelea Pyongyang katika hali nzuri.
Vilevile, Moon ameahidi kuliunganisha taifa hilo linalokabiliwa na ufisadi uliosababisha mtangulizi wake kushtakiwa bungeni na kuondolewa madarakani hivi karibuni. Kazi yake kubwa itakuwa kuimarisha uchumi.
Mtangulizi wake Park Geun-hye(65), ameshtakiwa rasmi kuhusiana na kashfa ya rushwa iliyopelekea kung'atuliwa kwake uongozini.

Previous
Next Post »