Mwanamfalme Phillip ambaye ndiye mumewe Malkia Elizabeth anajipunguzia majukumu ya utendaji kazi za kifalme, Kulingana na kasri la Buckingham palace.
Uamuzi huo ulichukuliwa na Mwanamfalme Phillip mwenyewe na unaungwa mkono na malikia Elizabeth kulingana na msemaji wa kasri hilo.
Philip ambaye atakuwa na umri wa miaka 96 mwezi Ujao atafanya kazi za kifalme kati ya sasa hadi mwezi Agosti lakini hatakubali mwaliko wowote.
- Malkia Elizabeth akosa ibada ya mwaka mpya
- Sarafu ya dhahabu ya $4m yaibiwa Ujerumani
- Watu milioni moja hawamtaki Trump Uingereza
Malkia Elizabeth ataendelea na majukumu yake yote ya kifalme kasri hiyo limesema.
Mwanamfalme huyo alifanya kazi siku 110 mwaka 2016 na hivyobasi kumfanya kuwa mwanachama wa 5 wa familia hiyo ya kifalme aliyekuwa na kazi nyingi.
''Ni kiongozi ,rais na mwanachama wa zaidi ya mashirika 780 na ataendelea kuhusishwa na mashirika hayo lakini hatochukua majukumu yenye kazi nyingi kupitia kuhudhuria hafla zao'', ilisema kasri ya Buckingham.
Katika taarifa msemaji huyo amesema kuwa ufalme huo utaendelea kuhudhuria hafla za umma mara kwa mara.
Sign up here with your email