MADEREVA SITA WA HALMASHAURI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE KWA KUGHUSHI VYETI - Rhevan Media

MADEREVA SITA WA HALMASHAURI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE KWA KUGHUSHI VYETI

Tokeo la picha la MAGARI YA HALMASHAURI


Lindi. Madereva sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wamehukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ya kughushi vyeti vya kidato cha nne na kujipatia ajira.
Hukumu hiyo imetolewa leo  na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kilwa, Gabriel Ngaeje baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani.
Madereva waliohukumiwa ni Juma  Sungura, Issa Abdurahman, Abdul Chubi, Dactuce Joseph, Ahmad Selemani na Abdallah Kilolopera.

Previous
Next Post »