Waogeleaji wa Tanzania wamekuwa ‘wakisota’ kwa miaka mingi kupata bwawa la kisasa la kuogelea lenye vifaa vya kutumia wakati wa kuchumpa ‘diving block’ na vifaa cha kurekodi muda cha elektroniki (Tough pad).
Kutokana na kukosekana kwa vifaa hivyo, waogeleaji wengi walikuwa wanalazimika kuwahi kuondoka nchini kwa ajili ya kuwahi kwenye mashindano kwa lengo la kuvifanyia mazoezi vya kisasa.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi amesema kuwa wamekubali klabu hiyo kuwekeza nchini kwa kujenga bwawa la kisasa lenye vifaa hivyo kwa lengo la kuboresha mchezo wa kuogelea hapa nchini.
Malinzi alisema kuwa wameridhika na uwasilishaji wa mpango wao huo na wanachotakwa kufanya ni kuanza mradi kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
“Huu mradi utawawezesha waogeleaji wetu kujifunza kwa muda mwingi kuliko hivi sasa ambapo wanfanya mazoezi kwenye mabwawa ya kuogelea ya shule tena kwa muda mfupi, Hamilton ni klabu kubwa yenye uzoefu wa kimataifa na wameweza kutoa waogeleaji wengi bora duniani, uwepo wao utachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya mchezo huo hapa nchini,” alisema Malinzi.
Mkurugenzi wa klabu hiyo, Christopher Tidey alisema kuwa wana mipango mingi ya kuendeleza mchezo huo na michezo mingine kwa ujumla.
“Klabu yetu ni kubwa yenye historia ya nzuri Mashriki ya Kati, tunawashukuru sana klabu ya Dar Swim Club (DSC) kwa kuwa mshirika nasi na maka sasa kupata ushirikiano mzuri na serikali,” alisema Tidey.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Hamilton Aquatics, Phillippa Clark amesema kuwa wamevutiwa na mazingira ya uwekezaji ya Tanzania na vile vile vipaji vya waogeleaji wake.
“Klabu ya DSC imekuwa ikishiriki mara kwa mara mashindano yetu na kuona vipaji, lakini historia inaonyesha kuwa waogeleaji hao wanafanya mazoezi bila ya kuwa na vifaa bora lakini kwa vipaji vyao, wameweza kufanya vyema, hebu fikiria kama watapata vifaa bora na kufanya mazoezi kwa muda mrefu, naamini watafanya vyema zaidi na kuleta medali za Olimpiki.
Sign up here with your email