KIFO CHA WAZIRI SOMALIA : MKAGUZI WA HESABU AFUTWA KAZI - Rhevan Media

KIFO CHA WAZIRI SOMALIA : MKAGUZI WA HESABU AFUTWA KAZI

Waziri Abbas alipigwa risasi kimakosa na mlinzi wa mkaguzi wa hesabu nchini Somalia
Image captionWaziri Abbas alipigwa risasi kimakosa na mlinzi wa mkaguzi wa hesabu nchini Somalia
Mkaguzi wa hesabu za serikali nchini Somalia ambaye mlinzi wake alimpiga risasi na kumuua waziri mwenzake katika kisa cha kimakosa amefutwa kazi.
Hatahivyo Nur Farah Jimale amekataa kuondoka afisini akisema hatua hiyo ni lazimi ipitishwe na bunge.
Waziri Abas Abdullahi Siraji ambaye ni mbunge mdogo zaidi nchini Somalia alipigwa risasi karibu na ikulu ya rais siku ya Jumatano baada ya walinzi kudhania kimakosa kwamba alikuwa mlipuaji wa kujitoa muhanga.
Kulingana na mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi sasa rais wa Somalia anataka hatua kuchukuliwa kufuatia kifo cha waziri huyo.
Lakini hatua yake ya kwanza imezua utata.
Baraza la mawaziri la Somalia liliidhinisha mpango wa waziri mkuu kumpiga kalamu mkaguzi huyo wa hesabu za serikali huku uchunguzi ukianzishwa kufuatia kifo cha waziri huyo.
Lakini bwana Jimale anasisitiza kwamba njia ya pekee ya kumuondoa afisini ni kupitia thuluthi mbili ya wabunge kuunga mkono hoja ya kumuondoa akinukuu sheria zilizopo katika katiba iliopo.
Aliongezea kuwa yeye ni mfanyikazi wa taifa na sio wa waziri mkuu.
Somalia inaendeshwa na katiba ya muda ilioidhinishwa na viongozi wa Somalia 2012.
Katiba hiyo haijapigiwa kura ya maoni na raia kutokana na tishio la Alshabab.
Ukosefu wa sheria madhubuti unaweza kutoa changamoto kwa serikali mpya ambayo imekuwa afisini kwa takriban miezi mitatu pekee.
Previous
Next Post »