ENG. NGONYANI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI UYOVU- BWANGA. - Rhevan Media

ENG. NGONYANI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI UYOVU- BWANGA.

unnamed

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akipokea taarifa ya maendeleo kutoka kwa Mhandisi Mkazi Eng. Juma Msonge, kuhusu ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami wakati alipokagua barabara hiyo jana, mkoani Geita
A
Mhandisi Mkazi Eng. Juma Msonge, akitoa taarifa ya maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami jana, mkoani Geita kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani.
A 1
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa maelekezo kwa Mhadisi Mkazi Eng. Juma Msonge, baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami jana, mkoani Geita.
A 2
Sehemu ya barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami na Mkandarasi Synohdro, mkoani Geita. Hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 60.
A 3
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Geita, Eng. Harun Senkuku, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ambae alikuwa mkoani humo kwa ajili ya kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara yake.
…………….
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa Km 45 inayojengwa na Mkandarasi M/S Sinohydro Corporation.
Akizungumza mkoani Geita jana, mara baada ya kukagua  barabara hiyo ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo KM 112, Naibu Waziri Eng. Ngonyani amemtaka mkandarasi huyo kahakikisha wanamaliza sehemu iliyobakia kwa muda uliopangwa.
“Nimeridhishwa na kasi yenu, hakika mmepiga hatua sana kwani awali nilipopita kukagua barabara hii haikuwa hivi”, amesema Naibu Waziri Ngonyani.
Aidha,  Eng. Ngonyani, amewapongeza wasimamizi wa barabara ya Biharamulo – Bwanga kutoka wakala wa barabara nchini (TANROADS) kupitia kitengo chake maalum cha wahandisi washauri wazawa (TECU),  kwa kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi M/S Sinohydro Corporation  kujenga barabara hiyo kwa viwango vilivyomo kwenye mkataba.
Kwa upande wake, Mhandisi mkazi wa barabara hiyo Eng. Juma Msonge, amemhakikishia Waziri huyo kumaliza barabara hiyo kwa wakati.
Eng. Msonge ameongeza kuwa kwa sasa mradi huo umefika asilimia 60 ambapo mkandarasi anaendelea na kazi ya kuweka matabaka ya lami ambapo ameshaweka km 30 kati ya 45 zilizopo kwenye barabara hiyo.
Naibu waziri  Ngonyani, amemaliza ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Geita ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Previous
Next Post »