BWANA HARUSI ATIWA MBARONI KWA KUJAZA NDUGU FEKI UKUMBINI - Rhevan Media

BWANA HARUSI ATIWA MBARONI KWA KUJAZA NDUGU FEKI UKUMBINI

Picha inayohusiana
BWANA harusi mchina, amekamatwa na polisi na sasa yuko rumande, baada ya kuhadaa wakwe zake kuwa amealika wageni 200, kumbe ni uongo watu hao wote ni wasanii wa kulipwa ukumbini.

Alipatwa na msukosuko huo baada ya familia ya mkewe kugundua kuwa watu aliokuwa anadai ni marafiki na ndugu zake, aliwapa ‘mshiko’ ili kuhudhuria harusi.

Kwa mujibu wa gazeti moja la jimbo la Kaskazini, nchini China, Polisi walimkamata Liu Wang., wakati ulipotokea mjadala kwenye mgogoro uliozuka baina yake na wageni ambao ilibainika ni marafiki tu, ingawa haikuwekwa wazi uhusiano wake nao.

Sherehe zilipoanza, hakukuwepo dalili za wazazi wa Liu kuwepo na ndipo joto la msuguano likaanza kupanda.

Mmoja wa wageni hao waalikwa wanaolipwa, aliiambia televisheni moja ya Shaanxi kwenye kipindi kiitwacho ‘guests’ kwamba walilipwa Yuan 80 ambazo ni sawa na Dola za Marekani 12 au sawa na Shilingi 25,000 au Pauni tisa, ambayo ni sawa na Shilingi 28,000 kutoka kwa bwana harusi - Wang.

Walisema walilipwa kwa kila siku waliyotumika ili wajifanye kama wanandugu zake .

Pia inadaiwa kuwa watu hao ni pamoja na madereva wa teksi, wanafunzi na maswahiba wengine wa bwana harusi huyo, kupitia mtandao wa kijamii wa jukwaa la ‘WeChat walijadiliana naye gharama za malipo kwa ushiriki wao kwenye harusi.

Bibi harusi alisema kuwa, amemfahamu mumewe huyo kwa zaidi ya miaka mitatu, ingawa hakufahamu chochote kuhusu utapeli wake.
Bado haijafahamika kile Liu anachokificha, licha ya kwamba hakuvunja sheria za nchi.

Baadhi ya vyombo vya habari vilidai kuwa, muoaji huyo alikuwa anatoka katika jamii maskini na katika kuficha uhalisia wake, aliamua kutosema ukweli kwa jamaa zake walioko vijijini, wasifike kwenye harusi, akihisi angeaibika.

Televisheni ya Kanda inayomilikiwa na serikali Xibu Online, imesema kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi.
Previous
Next Post »