Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtumia salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kufuatia vifo vya wananafunzi, walimu na dereva wa Shule ya Msingi Lucky Vicent, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali leo asubuhi katika eneo la Rhotia Marera, wilayani Karatu mkoani Arusha.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa nakupa pole sana, nimepokea kwa mshtuko taarifa hii ya ajali iliyogharimu maisha ya watoto wetu, hakika hili ni pigo kwa Taifa zima, namuomba Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi,” amesema Ndugai na kuongeza:
“Natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao, Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu, vilevile nawaombea majeruhi wote wa ajali hiyo wapate uponyaji wa haraka.”
Sign up here with your email