Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewajibu rasmi Simba SC juu ya sakata lao la kupokwa pointi tatu za mezani walizopewa baada ya rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar wakidai kumcheza mchezaji Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano.
Kwa mujibu wa barua kutoka katika Bodi ya Ligi zimesema kuwa Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano wakati akicheza mchezo dhidi ya Simba uliofanyikia uwanja wa Kaitaba, Bukoba Aprili 2 mwaka huu.
"TFF ambayo ndiyo yenye dhamana ya usimamizi wa mpira nchini na ambayo ndiyo iliyokaimu madaraka kwa TPLB kuendesha ligi kuu iliitisha kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo ilichunguza kwa undani sakata hili na baada ya uchunguzi wao ambao walihoji watu mbalimbali, walituandikia kutujulisha kuwa wamebaini mchezaji Mohamed Fakhi anayelalamikiwa na Simba hakuwa na kadi 3 siku ya mchezo wa Kagera Sugara dhidi ya Simba hivyo alikuwa halali kucheza mchezo huo". Ilisema barua hiyo
Sign up here with your email