ALIYEKUWA MWANDISHI WA BABA WA TAIFA ALAZWA JKCI - Rhevan Media

ALIYEKUWA MWANDISHI WA BABA WA TAIFA ALAZWA JKCI



 Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa mwandishi wa Baba wa Taifa, marehemu Julius Nyerere, Paul Sozigwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na anaendelea vyema na matibabu.
Msemaji wa JKCI, Anna Nkinda alisema Sozigwa alipokewa hospitalini hapo Aprili 25 ,akiwa na hali mbaya.
Nkinda alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri, ikilinganishwa na walivyompokea.
Akielezea kinachomsumbua baba yake mtoto wa Mzee Sozigwa, Mchungaji Moses Sozigwa alisema tatizo la kwanza lililokuwa likimsumbua baba yao ni kupoteza kumbukumbu.
Mchungaji Sozigwa alisema baadaye ilikuja kubainika ana tatizo la moyo, madaktari walisema moyo wake umekuwa mkubwa.
“Tunasubiri vipimo vingine tufahamu zaidi kinachomsumbua, nafikiri vitatoka leo (jana)au kesho (leo) kwa sababu pia amekuwa akilalamika kuumwa tumbo,” alisema Mchungaji Moses Sozigwa.     







Previous
Next Post »