AGIZO LA RAIS MAGUFULI LALETA NEEMA TANESCO - Rhevan Media

AGIZO LA RAIS MAGUFULI LALETA NEEMA TANESCO

Tokeo la picha la TANESCO
Makao makuu ya Tanesco jijini Dar es Salaam. 

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Ilala limekusanya Sh2 bilioni kutoka katika taasisi za Serikali zilizokuwa zinadaiwa na shirika hilo.
Deni hilo limekusanywa tangu Rais John Magufuli atoe agizo la kulitaka shirika hilo kuwakatia umeme wadaiwa sugu.
Akizungumza leo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Ilala, Athanasius Nangali amesema wadaiwa sugu walikuwa wanadaiwa jumla ya Sh 7 bilioni.
Taasisi za Serikali zilikuwa zinadaiwa Sh 6 bilioni na sasa wamelipa Sh 2 bilioni na zimebaki Sh 4 bilioni.
"Tumeingia mkataba na taasisi za serikali wa namna ya kulipa madeni yao na makubaliano ni kuwa watamaliza deni lililobaki mwezi huu hadi mwezi ujao," amesema.








Previous
Next Post »