ADAIWA KUMUUA BIB YAKE KWA RISASI - Rhevan Media

ADAIWA KUMUUA BIB YAKE KWA RISASI



Sumbawanga. Mkazi wa Kijiji  cha Ilonga kata ya Mambwekoswe mkoani Rukwa, Sikiliel  Nampunje (55) amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mjukuu wake kutokana na migogoro ya mashamba.
Kaimu  Kamanda  wa  Polisi  Mkoa wa Rukwa, Polycarp Urio amesema tayari mtu huyo amekamatwa kwa mahojiano zaidi.
Taarifa zilizopatikana leo zinaeleza kwamba tukio limetokea juzi ambapo kijana alimuua bibi yake huyo kutokana na kwenda kwenye  uongozi  wa kata  hiyo  kudai  haki  yake kufuatia  koporwa mashamba  na  ndugu  zake.
Imeelezwa kuwa baada ya kijana huyo kusikia bibi yake amekwenda ofisi ya kata kudai haki yake ndipo alipomvizia njiani na kumpiga  risasi.
Mume wa marehemu aitwaye Abbas Kapunda alisema mkewe  alikumbwa  na mkasa  huo  wakati  akitoka kwenye shughuli zake za kilimo shambani na alikuwa akirejea nyumbani.
Amesema   baada  ya  kusikia  kelele  za  kuomba msaada  waliamua kuelekea   eneo  la  tukio  na  kumkuta mkewe  akiwa   anatokwa  na  damu eneo la kifuani ambapo walitoa taarifa   kwa  uongozi  wa  kijiji na kisha kumkimbiza katika zahanati ya kijiji ambako alifariki wakati akipatiwa matibabu.
Amesema chanzo  cha  kifo hicho ni mgogoro  wa  mashamba  ambayo  yalikuwa yakigombaniwa  na wanafamilia hao.









Previous
Next Post »