MWANDISHI MAARUFU KUKI GALLMANN APINGWA RISASI NA KUJERUHIWA KENYA - Rhevan Media

MWANDISHI MAARUFU KUKI GALLMANN APINGWA RISASI NA KUJERUHIWA KENYA

Kuki Gallmann
Haki miliki ya pichaAFP
Image captionHoteli ya kifahari inayomilikiwa na Bi Gallmann ilichomwa moto mwezi uliopita
Watu waliojihami na bunduki wamempiga risasi na kumjeruhi mwanamazingira na mwandishi mzoefu mzaliwa wa Italia, Kuki Gallmann.
Amepigwa risasi ya tumbo akiwa kwenye shamba lake kaunti ya Laikipia.
Mwezi uliopita makahawa wake wa kifahari uliteketezwa na watu wanaoshukiwa kuwa wafugaji.
Bi Gallmann, amekuwa mwenyeji wa Kenya tangu miaka ya sabini, na anafahamika zaidi kutokana na kitabu chake 'I Dreamed of Africa'.
Filamu ya kitabu hicho pia ilitolewa, mhusika mkuu, akiwa mwigizaji maarufu wa Marekani , Kim Basinger.
Burned Mukutan lodgeHaki miliki ya pichaTHE STAR, KENYA
Image captionMwezi uliopita makahawa wa Bi Gallmann uliteketezwa na wafugaji
map
Image captionLaikipia
Previous
Next Post »