WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA WAJITOKEZA KWA KASI KUPATA UDUMA YA KUPIMA AFYA ZAO BURE KATIKA WIKI YA WANAWAKE DUNIANI - Rhevan Media

WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA WAJITOKEZA KWA KASI KUPATA UDUMA YA KUPIMA AFYA ZAO BURE KATIKA WIKI YA WANAWAKE DUNIANI

 Baadhi ya wananchi  wakichukuliwa vipimo vya afya na madaktari kutoka kcmc pamoja na Mounti meru Hospital ikiwa ni huduma inayotolewa bure katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid katika wiki ya wanawake duniani  ambayo kwa mkoa wa Arusha imeandaliwa na Phide intantament
 Baadhi ya wananchi wakiwa katika mstari wakisubiri kuchukuliwa vipimo vya magonjwa mbalimbali bure yakiwemo ,Kisukari ,Presha,Kansa  ,Ukimwi na mengineyo
mmoja wa madaktari akiendelea kupima mara baada ya kuchukuwa vipimo vya wagonjwa ndani  viwanja vya Sheikh Amri Abeid
 
 Na Woinde Shizza,Arusha
Maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani yameanza rasmi mkoani Arusha  ambapo wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wamepata fursa ya kupata huduma ya kupima magonjwa mbalimbali bure
 
zoezi hilo ambalo limeanza leo jijini hapa katika kiwanja cha sheikh Amri Abeid limeonekana kuwavuta wananchi wengi kwani zaidi ya wananchi 100 wamejotokeza kupima afya zao   bure katika viwanja hivyo
 
Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa maathimisho hayo ya wiki ya wananwake duniani kwa mkoa wa Arusha mkurugenzi wa Phide Intantament Phidesia Mwakitalima alisem akuwa muamko ni mzuri na wananchi wameanza kujitokeza kwa wingi 
 
Alisema kuwa pamoja ni siku ya kwanza tu lakini zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao  hivyo ni jambo zuri mno 
 
Alisema kumekuwepo na tabia ya wananchi wengi kutokuwa na  tabia ya kupima afya zao hadi pale wanapoumwa kitu ambacho sio kizuri na kuwataka wananchi  kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara
Zoezi hili la kupima afya limeanza leo na linatarajiwa kumalizika march nane na huduma za kupima magonjwa mbalimbali na ushauri wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kuchangia damu unatolew bure hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutumia fursa hiii ili kujua afya yake
Previous
Next Post »