MEYA WA JIJI LA ARUSHA CALIST LAZARO AMPONGEZA MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA KWA KUFANIKISHA KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA - Rhevan Media

MEYA WA JIJI LA ARUSHA CALIST LAZARO AMPONGEZA MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA KWA KUFANIKISHA KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia akiongea na waandishi wa habari
 
Na Woinde Shizza,Arusha
Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametoa pongezi kwa
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia, timu ya wataalam wa Jiji
hilo pamoja na baraza la madiwani kwa kufanikisha zoezi la kujenga
vyumba vya madarasa, madawati kwakutumia mapato ya ndani pasipo
kuchangisha wananchi 
Pongezi hizo zilitolewa juzi Jijini hapa kwenye Baraza la
Kawaida la Madiwani lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali
pamoja na wananchi wa Jiji la Arusha.
Lazaro alisema  Jiji limefanikiwa kuondoa kero ya uhaba wa
dada rasa, madawati bila kuwachangisha wananchi ,jambo ambalo limesaidia
wanafunzi kuanza masoma kwa wakati.
Alisema watoto wote wa shule za msingi wameweza kuingia
shuleni na kukaa kwenye madawati kwani Jiji wamefanikiwa kujenga
madarasa 56,madawati 1250,madarasa 25 ya sekondari pasipo kuomba fedha
sehemu nyingine pamoja na kuwachangisha wazazi.
“Tunakupongeza wewe Mkurugenzi wa Jiji letu pamoja na timu
ya wataalam wa Jiji pamoja na madiwani kwa kuhakikisha Jiji la Arusha
linaondokana na kero ya uhaba huo wa madawati ambao awali ulikuwa
ukisumbua wanafunzi “
Naye Mkurugenzi wa Jiji hilo, Kihamia alishukuru kwa baraza
hilo kutambua kazi anazozifanya za maendeleo na kuomba ushirikiano
zaidi kwa madiwani hao ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi.
Katika baraza hilo Pia kulikuwa na wawakilishi wa idara za
serikali walioalikwa ili kutoa taarifa za utendaji kazi kwa baraza hilo
ndipo hoja za tatizo la maji ilipoibuka kutoka kwa madiwani ambao
walisema inashangaza Jiji la Arusha kuwa ni Jiji la Kitalii lakini bado
wananchi wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji huku wengine wakikosa
kupata maji na bili kuwa kubwa.
Akijibu hoja hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na
Taka  (AUWSA) Mhandisi, Ruth Koya  alisema mamlaka hiyo inashughulikia
kero hiyo ya maji na kutoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka
hiyo ili kuweza kutatua changamoto ya maji Jiji la Arusha
Pia suala  la ukodishwaji maduka ya biashara liliibuliwa na
madiwani  katika maswali ya papo kwa papo kwa Meya na Mkurugenzi kuwa
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anangilia mchakato wa utoaji
zabuni za maduka . ambapo Mkurugenzii wa Jiji , Kihamia alilazimika
kukanusha uzumi huo kwa kusema kuwa Rc, Gambo anaweza kuingilia maamuzi
ya baraza hilo kwa maslahi ya mkoa kwa mamlaka aliyonayo.
Pia alisisitiza kuwa Rc Gambo alikutana na wajenzi hao wa
maduka na wafanyabiashara ili kujua changamoto zinazowakabili na
kuzitatua kwa maslahi mapana ya maendeleo.
 Awali Jiji la Arusha liliingia katika mvutano wa
wafanyabishara waliopangisha katika majengo ya jiji tatizo liliopatiwa
ufumbuzi na Mkuu wa Mkoa hivi karibuni.
Previous
Next Post »