Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai Akizungumza na Watendaji, Viongozi na wafuasi wa chama hicho katika mwendelezo ya ziara ya kuimarisha uhai wa Chama kuelekea uchaguzi wa taasisi hiyo na jumuiya zake Katika Jimbo la Jang’ombe iliyofanyika katika Tawi la Matarumbeta.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai ameuagiza Uongozi wa Wilaya ya Mjini kichama kichama kufuatilia sababu za kufukuzwa kwa Viongozi Wawili wa Jimbo la Jang’ombe na kutafuta na kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo haraka kupitia miongozo na kanuni za Katiba ya Chama hicho.
Alisema ina utaratibu wa kushughulikia migogoro ndani ya Chama na Jumuiya zake kwa ngazi mbali mbali kwa kufuata misingi ya Katiba hivyo ni lazima kasoro zinazojitokeza ndani ya taasisi hiyo ni lazima zitatuliwe kwa utaratibu uliowekwa na sio matakwa binafsi ya baadhi ya Viongozi.
Vuai alisema kwa mujibu wa Kanuni za masuala ya Uongozi Kamati za Siasa za Majimbo hazina mamlaka ya kuwafukuza ama kuwaondosha katika nafasi za uongozi kwa ngazi za Majimbo badala yake wanatakiwa kufanya vikao vya kikatiba kuwajadili watu wanaotuhumiwa na kuwasilisha mapendekezo yao kwa ngazi ya wilaya ili ijadili na kuchukua hatua stahiki kwa kuzingatia taratibu za CCM.
Agizo hilo limetokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa viongozi wawili waliovuliwa nafasi za uongozi katika Jimbo hilo kumueleza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Nd. Vuai Ali Vuai kuwa wameonewa kwani wamefukuzwa wakiwa hawajui kosa linalowakabili na bila kupewa nafasi za kujieleza.
Akitoa ufafanuzi juu ya Malalamiko hayo Naibu Katibu Mkuu huyo aliutaka uongozi wa Wilaya hiyo kufuatilia kwa kina mgogoro huo ili umalize bila kuathiri uongozi wa Jimbo hilo, na kuwasihi Viongozi, Watendaji na Wanachama kusoma Katiba ya CCM na kanuni za chama hicho kwa lengo la kujikumbusha mambo ya msingi yatakayosaidia kuepuka kasoro zisizokuwa za lazima.
“Chama Cha Mapinduzi kinaongozwa kwa misingi ya kikatiba na maamuzi mbali mbali yanayofanyika yanafuata muongozo huo na kila ngazi imepewa majukumu yake kulingana na kanuni zetu hivyo nakukumbusheni kuwa viongozi tuwe makini kuhakikisha tunasoma kwa makini Katiba na Kanuni zinazotuongoza.
Lakini tusikubali kugawanyika kwa tofauti ndogo ndogo zinazojitokeza kama changamoto ndani ya Chama chetu na tunaposhutumiana hadharani tunavunja utaratibu unaotuongoza ndani ya taasisi yetu”, alisema Vuai na kusisitiza kuwa Umoja, Upendo na ushirikiano ndani ya jimbo hilo na CCM kwa ujumla ndio siri ya mafanikio.
Hata hivyo aliwambia wanachama hao kuwa mabadiliko ya kimuundo yanayofanyika ndani ya Taasisi hiyo yanalenga kujenga Chama chenye nguvu za kiuchumi utakaotokana na matumizi mazuri ya rasilimali zake kwa maslahi ya wanachama wote.
Kupitia ziara hiyo aliwakumbusha viongozi na watendaji wa Chama hicho kusimamia vizuri miradi ya CCM ili isaidie shughuli za kiutendaji na kuwanufaisha wanachama wote badala ya watu wachache.
Akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini, Nd. Juma Fakih Choum alimueleza Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa baada ya kupata malalamiko ya kufukuzwa kwa viongozi hao Wilaya hiyo ilichukua hatua za kuuagiza uongozi wa jimbo kukutana pamoja katika kikao ili wajadiliane na kutafuta ufumbuzi wa kumaliza mzozo huo.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema ndani ya Wilaya hiyo wamejiandaa kikamilifu kushiriki katika uchaguzi wa Chama na Jumuiya zake ili kupata viongozi na watendaji imara wa ngazi mbali mbali watakaoweza kusimamia mikakati ya ushindi mwaka 2020.
Sign up here with your email