Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna mstaafu Zelote Stephen amelipongeza jeshi la polisi Mkoani Rukwa kwa kufanikiwa kukamata kilo mbili za madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni heroin na lori la scania lililosheheni pombe za viroba lililokuwa likitokea Mbeya na kuingia Rukwa kwa njia za panya.
Jeshi la polisi Mkoani Rukwa limemtia nguvuni Mtuhumiwa
wa madawa ya kulevya Linus Tenda Kamwezi (50) mfanyabiashara mkazi wa kizwite
katika manispaa ya sumbawanga aliyebainika kuyaficha madawa hayo katika maua
yaliyokuwa yamezunguka nyumba yake.
“Pamoja na kwamba mna-resource ndogo lakini kazi
mnayoifanya ni kubwa sana, nawapongeza kwa kitendo hiki na mwendelee kushika
kamba hiyo hiyo dhidi ya vita hii ya madawa ya kulevya ambayo si ya jeshi la
polisi peke yao bali ni la wananchi wote wa nchi ya Tanzania,” Zelote Stephen
alieleza.
Sambamba na hilo Kamanda wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando
alifafanua kuwa watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa na
lori aina ya Scania lililosheheni pombe zenye vifungashio vya nailon maarufu pombe
za viroba wakitokea Mkoani Mbeya kuelekea Rukwa.
Sign up here with your email