SHETANI WA WANYAMA PORI AFUNGWA MIAKA 12 JELA - Rhevan Media

SHETANI WA WANYAMA PORI AFUNGWA MIAKA 12 JELA

Boniface Matthew Maliango au Shetani alipatikana na pembe 118
Image captionBoniface Matthew Maliango au Shetani alipatikana na pembe 118
Mmoja wa wawindaji hatari zaidi wa wanyama pori barani Afrika ambye pia anafahamika kama "Shetani" amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela nchini Tanzania.
Boniface Matthew Maliango, ambaye amekwepa kukamatwa mara kadha alitiwa mbaroni mwezi Oktoba.
Mwandishi wa habari ambaye alikuwa akifuatilia kesi hiyo kwenye mji wa Dodoma, anasema kuwa muwindaji huyo hatari alipatikana na pembe 118 zenye thamani ya zaidi ya dola 860,000.
Alizungumziwa kwenye makala moja wa Netflix, yanayofahamika kama Ivory Game, yaliyotengenezwa na mcheza filamu Leonardo DiCaprio.
Boniface Matthew Maliango au Shetani ahukumia kifungo cha Miaka 12 jelaHaki miliki ya pichaFACEBOOK PAMS FOUNDATION
Image captionBoniface Matthew Maliango au Shetani ahukumia kifungo cha Miaka 12 jela
Previous
Next Post »