UFA YAJA NA KOMBE LA FA UBUNGO - Rhevan Media

UFA YAJA NA KOMBE LA FA UBUNGO


Dar es Salaam. Chama cha soka Ubungo (UFA)  kimetoa ratiba ya mashindano ya FA kwa timu za wilaya hiyo, yatakayoanza Machi 11.
Katibu mkuu wa UFA,  Frank Mchaki alisema kuwa mashindano hayo yatafanyika kwenye viwanja viwili vya Kinesi na Shule ya Sekondari Matosa.
"Kwenye mechi ya ufunguzi, Faru Dume watacheza na Mugabe FC kwenye Uwanja wa Kinesi wakati siku inayofuata Maji Chumvi watacheza na Matosa," alisema Mchaki.
Hii ni mara ya kwanza kwa chama cha soka kwa wilaya nchini kuandaa mashindano hayo.
Previous
Next Post »