SUDAN KUSINI HATARINI KUINGIA MAUAJI YA KIMBARI - UN - Rhevan Media

SUDAN KUSINI HATARINI KUINGIA MAUAJI YA KIMBARI - UN

UN
Image captionWanajeshi wa Sudan Kusini
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema Sudan kusini iko hatarini kuingia kwenye mauaji ya kimbari.Ripoti hii ni matokeo ya uchunguzi wa miezi saba kuhusu masuala ya haki za binadamu nchini humo.Kumekuwepo na shutuma za ukiukwaji wa haki za kibinadamu zinazotekelezwa na wanajeshi wa pande zote mbili kwa kufanya vitendo vya mauaji, ubakaji na uporaji.
Watu milioni moja na nusu wameikimbia nchi hiyo kwenda nchi jirani katika kipindi cha miaka mitatu ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na sasa ni kwa sababu ya njaa pia, Mgogoro huu wa kisiasa umeanza kwa kasi kugawanya jeshi katika misingi ya kikabila na maeneo ya mji wa Yei.
Wakati ,Umoja wa mataifa umeonya hatari ya kutokea mauaji ya kimbari ,Brigedia jenerali Chol Deng Chol amekanusha shutuma hizo.
''hakuna vitendo vya mauaji au ubakaji, na kama kuna mwanajeshi anafanya hivyo napaswa kumkamata haraka sana, tunaopambana nao ni waasi hapo ndipo mauaji hutokea, wanaonusurika hudai kuwa raia wanauawa na wanajeshi, lakini hatuwaui raia wetu nchini mwetu''
Previous
Next Post »